Zaburi 65:6
Psalms 65:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
uliyeumba milima kwa uwezo wako, ukiwa umejivika nguvu,
Psalms 65:6 in English
Psalms 65:6 · Berean Standard Bible
You formed the mountains by Your power, having girded Yourself with might.
Context
4Heri wale uliowachagua
na kuwaleta karibu ili waishi katika nyua zako!
Tunashibishwa kwa mema ya nyumba yako,
mema ya Hekalu lako takatifu. 5Unatujibu kwa matendo ya kushangaza ya haki,
Ee Mungu Mwokozi wetu,
tumaini la miisho yote ya duniani
na la bahari zilizo mbali sana, 6uliyeumba milima kwa uwezo wako,
ukiwa umejivika nguvu, 7uliyenyamazisha dhoruba za bahari,
ngurumo za mawimbi yake,
na ghasia za mataifa. 8Wale wanaoishi mbali sana
wanaogopa maajabu yako,
kule asubuhi ipambazukiapo
na kule jioni inakofifilia
umeziita nyimbo za furaha.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.