Zaburi 64:8
Psalms 64:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Atageuza ndimi zao wenyewe dhidi yao na kuwaleta kwenye maangamizi; wote wawaonao watatikisa vichwa vyao kwa dharau.
Psalms 64:8 in English
Psalms 64:8 · Berean Standard Bible
They will be made to stumble, their own tongues turned against them. All who see will shake their heads.
Context
6Hufanya shauri baya la dhuluma na kusema,
“Tumebuni mpango mkamilifu!”
Hakika nia na moyo wa mwanadamu vina hila. 7Bali Mungu atawapiga kwa mishale,
nao ghafula wataangushwa. 8Atageuza ndimi zao wenyewe dhidi yao
na kuwaleta kwenye maangamizi;
wote wawaonao watatikisa vichwa vyao
kwa dharau. 9Wanadamu wote wataogopa,
watatangaza kazi za Mungu
na kutafakari yale aliyoyatenda. 10Wenye haki na wafurahi katika Bwana,
na wakimbilie kwake;
wanyofu wote wa moyo na wamsifu yeye!
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.