Native Bible

Psalms 50:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mungu wetu anakuja na hatakaa kimya, moto uteketezao unamtangulia, akiwa amezungukwa na tufani kali.

Psalms 50:3 in English

Psalms 50:3 · Berean Standard Bible

Our God approaches and will not be silent! Consuming fire precedes Him, and a tempest rages around Him.

Context

1Mwenye Nguvu, Mungu, Bwana, asema na kuiita dunia, tangu mawio ya jua hadi mahali pake liendapo kutua. 2Kutoka Sayuni, penye uzuri mkamilifu, Mungu anaangaza. 3Mungu wetu anakuja na hatakaa kimya, moto uteketezao unamtangulia, akiwa amezungukwa na tufani kali. 4Anaziita mbingu zilizo juu, na nchi, ili aweze kuwahukumu watu wake: 5“Nikusanyieni watu wangu waliowekwa wakfu, waliofanya agano nami kwa dhabihu.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.