Zaburi 45:7
Psalms 45:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Unaipenda haki na kuchukia uovu; kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekuweka juu ya wenzako, kwa kukupaka mafuta ya furaha.
Psalms 45:7 in English
Psalms 45:7 · Berean Standard Bible
You have loved righteousness and hated wickedness; therefore God, your God, has anointed you above your companions with the oil of joy.*
Context
5Mishale yako mikali na ichome mioyo ya adui za mfalme,
mataifa na yaanguke chini ya nyayo zako. 6Ee Mungu, kiti chako cha enzi
kitadumu milele na milele,
fimbo ya utawala wa haki
itakuwa fimbo ya utawala wa ufalme wako. 7Unaipenda haki na kuchukia uovu;
kwa hiyo Mungu, Mungu wako,
amekuweka juu ya wenzako,
kwa kukupaka mafuta ya furaha. 8Mavazi yako yote yana harufu nzuri
ya manemane, udi na mdalasini;
kutoka kwenye majumba ya kifalme
yaliyopambwa kwa pembe za ndovu,
sauti za vinanda vya nyuzi
zinakufanya ufurahi. 9Binti za wafalme ni miongoni mwa wanawake wako waheshimiwa;
kuume kwako yupo bibi arusi malkia aliyevaa dhahabu ya Ofiri.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.