Zaburi 31:21
Psalms 31:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Atukuzwe Bwana, kwa kuwa amenionyesha upendo wake wa ajabu nilipokuwa katika mji uliozingirwa.
Psalms 31:21 in English
Psalms 31:21 · Berean Standard Bible
Blessed be the LORD, for He has shown me His loving devotion in a city under siege.
Context
19Tazama jinsi ulivyo mkuu wema wako,
uliowawekea akiba wakuchao,
ambao huwapa wale wakukimbiliao
machoni pa watu. 20Unawahifadhi katika uvuli wa uwepo wako
kutokana na hila za wanadamu;
katika makao yako huwaweka salama
kutokana na ndimi za mashtaka. 21Atukuzwe Bwana,
kwa kuwa amenionyesha upendo wake wa ajabu
nilipokuwa katika mji uliozingirwa. 22Katika hofu yangu nilisema,
“Nimekatiliwa mbali na macho yako!”
Hata hivyo ulisikia kilio changu
ukanihurumia nilipokuita unisaidie. 23Mpendeni Bwana ninyi watakatifu wake wote!
Bwana huwahifadhi waaminifu,
lakini wenye kiburi huwalipiza kikamilifu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.