Native Bible

Psalms 31:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Siku za maisha yangu ziko mikononi mwako, uniokoe mikononi mwa adui zangu na wale wanifuatiao.

Psalms 31:15 in English

Psalms 31:15 · Berean Standard Bible

My times are in Your hands; deliver me from my enemies and from those who pursue me.

Context

13Kwa maana nimesikia maneno niliyosingiziwa na wengi; vitisho viko pande zote; kwa kuwa wamefanya mashauri dhidi yangu, na kula njama kuniua. 14Lakini mimi ninakutumaini wewe peke yako, Ee Bwana; nimesema, “Wewe ndiwe Mungu wangu.” 15Siku za maisha yangu ziko mikononi mwako, uniokoe mikononi mwa adui zangu na wale wanifuatiao. 16Mwangazie mtumishi wako uso wako, uniokoe kwa ajili ya upendo wako usiokoma. 17Usiniache niaibike, Ee Bwana, kwa maana nimekulilia wewe, bali waovu waaibishwe na kunyamazishwa Kuzimu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.