Zaburi 31:13
Psalms 31:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa maana nimesikia maneno niliyosingiziwa na wengi; vitisho viko pande zote; kwa kuwa wamefanya mashauri dhidi yangu, na kula njama kuniua.
Psalms 31:13 in English
Psalms 31:13 · Berean Standard Bible
For I hear the slander of many; there is terror on every side. They conspire against me and plot to take my life.
Context
11Kwa sababu ya adui zangu wote,
nimedharauliwa kabisa na jirani zangu,
hata kwa rafiki zangu nimekuwa tisho,
wale wanionao barabarani hunikimbia. 12Nimesahaulika miongoni mwao kama mtu aliyekufa,
nimekuwa kama chombo cha mfinyanzi kilichovunjika. 13Kwa maana nimesikia maneno niliyosingiziwa na wengi;
vitisho viko pande zote;
kwa kuwa wamefanya mashauri dhidi yangu,
na kula njama kuniua. 14Lakini mimi ninakutumaini wewe peke yako, Ee Bwana;
nimesema, “Wewe ndiwe Mungu wangu.” 15Siku za maisha yangu ziko mikononi mwako,
uniokoe mikononi mwa adui zangu
na wale wanifuatiao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.