Zaburi 22:21
Psalms 22:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Niokoe kutoka kinywani mwa simba, niokoe kutoka pembe za mafahali mwitu.
Psalms 22:21 in English
Psalms 22:21 · Berean Standard Bible
Save me from the mouth of the lion; at the horns of the wild oxen You have answered me!
Context
19Lakini wewe, Ee Bwana,
usiwe mbali.
Ee Nguvu yangu,
uje haraka unisaidie. 20Okoa maisha yangu na upanga,
uhai wangu wa thamani kutoka nguvu za mbwa. 21Niokoe kutoka kinywani mwa simba,
niokoe kutoka pembe za mafahali mwitu. 22Nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu,
katika kusanyiko nitakusifu wewe. 23Ninyi ambao mnamcha Bwana, msifuni!
Ninyi nyote wazao wote wa Yakobo, mheshimuni yeye!
Mcheni yeye, ninyi wazao wote wa Israeli!
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.