Native Bible

Psalms 22:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ninyi ambao mnamcha Bwana, msifuni! Ninyi nyote wazao wote wa Yakobo, mheshimuni yeye! Mcheni yeye, ninyi wazao wote wa Israeli!

Psalms 22:23 in English

Psalms 22:23 · Berean Standard Bible

You who fear the LORD, praise Him! All descendants of Jacob, honor Him! All offspring of Israel, revere Him!

Context

21Niokoe kutoka kinywani mwa simba, niokoe kutoka pembe za mafahali mwitu. 22Nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu, katika kusanyiko nitakusifu wewe. 23Ninyi ambao mnamcha Bwana, msifuni! Ninyi nyote wazao wote wa Yakobo, mheshimuni yeye! Mcheni yeye, ninyi wazao wote wa Israeli! 24Kwa maana hakupuuza wala kudharau mateso ya aliyeonewa; hakumficha uso wake bali alisikiliza kilio chake ili amsaidie. 25Kwako wewe hutoka kiini cha sifa zangu katika kusanyiko kubwa, nitatimiza nadhiri zangu mbele ya wale wakuchao wewe.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.