Zaburi 19:5
Psalms 19:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
linafanana na bwana arusi akitoka chumbani mwake, kama shujaa afurahiavyo kukamilisha kushindana kwake.
Psalms 19:5 in English
Psalms 19:5 · Berean Standard Bible
Like a bridegroom emerging from his chamber, like a champion rejoicing to run his course,
Context
3Hakuna msemo wala lugha,
ambapo sauti zao hazisikiki. 4Sauti yao imeenea duniani pote,
nayo maneno yao yameenea
hadi miisho ya ulimwengu.
Katika mbingu amepiga hema kwa ajili ya jua, 5linafanana na bwana arusi
akitoka chumbani mwake,
kama shujaa afurahiavyo
kukamilisha kushindana kwake. 6Huchomoza upande mmoja wa mbingu,
na kufanya mzunguko wake
hadi upande mwingine.
Hakuna kilichojificha joto lake. 7Sheria ya Bwana ni kamilifu,
ikihuisha nafsi.
Shuhuda za Bwana ni za kuaminika,
zikimpa mjinga hekima.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.