Native Bible

Psalms 17:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hatua zangu zimeshikamana na njia zako; nyayo zangu hazikuteleza.

Psalms 17:5 in English

Psalms 17:5 · Berean Standard Bible

My steps have held to Your paths; my feet have not slipped.

Context

3Ingawa unauchunguza moyo wangu na kunikagua usiku, ingawa umenijaribu, hutaona chochote. Nimeamua kwamba kinywa changu hakitatenda dhambi. 4Kuhusu matendo ya wanadamu: kwa neno la midomo yako, nimejiepusha na njia za wenye jeuri. 5Hatua zangu zimeshikamana na njia zako; nyayo zangu hazikuteleza. 6Ee Mungu, ninakuita, kwa kuwa utanijibu, nitegee sikio lako na usikie ombi langu. 7Uonyeshe ajabu ya upendo wako mkuu, wewe uokoaye kwa mkono wako wa kuume wale wanaokukimbilia kutokana na adui zao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.