Zaburi 144:11
Psalms 144:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nikomboe na uniokoe kutoka mikononi mwa wageni ambao vinywa vyao vimejaa uongo, na mikono yao ya kuume ni midanganyifu.
Psalms 144:11 in English
Psalms 144:11 · Berean Standard Bible
Set me free and rescue me from the grasp of foreigners, whose mouths speak falsehood, whose right hands are deceitful.
Context
9Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mpya,
kwa zeze yenye nyuzi kumi nitakuimbia, 10kwa Yule awapaye wafalme ushindi,
ambaye humwokoa Daudi, mtumishi wake kutokana na upanga hatari. 11Nikomboe na uniokoe
kutoka mikononi mwa wageni
ambao vinywa vyao vimejaa uongo,
na mikono yao ya kuume ni midanganyifu. 12Kisha wana wetu wakati wa ujana wao
watakuwa kama mimea iliyotunzwa vizuri,
binti zetu watakuwa kama nguzo zilizoviringwa
kurembesha jumba la kifalme. 13Ghala zetu zitajazwa
aina zote za mahitaji.
Kondoo zetu watazaa kwa maelfu,
kwa makumi ya maelfu katika mashamba yetu;
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.