Native Bible

Psalms 142:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wakati roho yangu inapozimia ndani yangu, wewe ndiwe unajua njia zangu. Katika njia ninayopita watu wameniwekea mtego.

Psalms 142:3 in English

Psalms 142:3 · Berean Standard Bible

Although my spirit grows faint within me, You know my way. Along the path I travel they have hidden a snare for me.

Context

1Namlilia Bwana kwa sauti, nainua sauti yangu kwa Bwana anihurumie. 2Namimina malalamiko yangu mbele zake, mbele zake naeleza shida zangu. 3Wakati roho yangu inapozimia ndani yangu, wewe ndiwe unajua njia zangu. Katika njia ninayopita watu wameniwekea mtego. 4Tazama kuume kwangu na uone, hakuna hata mmoja anayejihusisha nami. Sina kimbilio, hakuna anayejali maisha yangu. 5Ee Bwana, nakulilia wewe, nasema, “Wewe ni kimbilio langu, fungu langu katika nchi ya walio hai.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.