Native Bible

Psalms 12:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Bwana na akatilie mbali midomo yote ya hila na kila ulimi uliojaa majivuno,

Psalms 12:3 in English

Psalms 12:3 · Berean Standard Bible

May the LORD cut off all flattering lips and every boastful tongue.

Context

1Bwana tusaidie, kwa kuwa wacha Mungu wametoweka; waaminifu wametoweka miongoni mwa wanadamu. 2Kila mmoja humwambia jirani yake uongo; midomo yao ya hila huzungumza kwa udanganyifu. 3Bwana na akatilie mbali midomo yote ya hila na kila ulimi uliojaa majivuno, 4ule unaosema, “Kwa ndimi zetu tutashinda; midomo ni mali yetu, bwana wetu ni nani?” 5“Kwa sababu ya uonevu wa wanyonge na kulia kwa uchungu kwa wahitaji, nitainuka sasa,” asema Bwana. “Nitawalinda kutokana na wale wenye nia mbaya juu yao.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.