Zaburi 112:3
Psalms 112:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nyumbani mwake kuna mali na utajiri, haki yake hudumu milele.
Psalms 112:3 in English
Psalms 112:3 · Berean Standard Bible
Wealth and riches are in his house, and his righteousness endures forever.
Context
1Msifuni Bwana.
Heri mtu yule amchaye Bwana,
mtu yule apendezwaye sana na amri zake. 2Watoto wake watakuwa wenye uwezo katika nchi,
kizazi cha watu waadilifu kitabarikiwa. 3Nyumbani mwake kuna mali na utajiri,
haki yake hudumu milele. 4Hata gizani nuru humzukia mtu mwadilifu,
yule mwenye rehema, huruma na haki. 5Mema yatamjia mtu yule aliye mkarimu na mwenye kukopesha bila riba,
anayefanya mambo yake kwa haki.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.