Native Bible

Psalms 104:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Huzifanya pepo kuwa wajumbe* wake, miali ya moto watumishi wake.

Psalms 104:4 in English

Psalms 104:4 · Berean Standard Bible

He makes the winds His messengers, flames of fire His servants.*

Context

2Amejifunika katika nuru kama vile kwa vazi, amezitandaza mbingu kama hema 3na kuziweka nguzo za orofa yake juu ya maji. Huyafanya mawingu kuwa gari lake, na hupanda kwenye mbawa za upepo. 4Huzifanya pepo kuwa wajumbe* wake, miali ya moto watumishi wake. 5Ameiweka dunia kwenye misingi yake, haiwezi kamwe kuondoshwa. 6Uliifunika kwa kilindi kama kwa vazi, maji yalisimama juu ya milima.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.