Native Bible

Psalms 104:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

na kuziweka nguzo za orofa yake juu ya maji. Huyafanya mawingu kuwa gari lake, na hupanda kwenye mbawa za upepo.

Psalms 104:3 in English

Psalms 104:3 · Berean Standard Bible

laying the beams of His chambers in the waters above, making the clouds His chariot, walking on the wings of the wind.

Context

1Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Ee Bwana Mungu wangu, wewe ni mkuu sana, umejivika utukufu na enzi. 2Amejifunika katika nuru kama vile kwa vazi, amezitandaza mbingu kama hema 3na kuziweka nguzo za orofa yake juu ya maji. Huyafanya mawingu kuwa gari lake, na hupanda kwenye mbawa za upepo. 4Huzifanya pepo kuwa wajumbe* wake, miali ya moto watumishi wake. 5Ameiweka dunia kwenye misingi yake, haiwezi kamwe kuondoshwa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.