Native Bible

Psalms 100:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu. Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake; sisi tu watu wake, kondoo wa malisho yake.

Psalms 100:3 in English

Psalms 100:3 · Berean Standard Bible

Know that the LORD is God. It is He who made us, and we are His;* we are His people, and the sheep of His pasture.

Context

1Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote. 2Mwabuduni Bwana kwa furaha; njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe. 3Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu. Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake; sisi tu watu wake, kondoo wa malisho yake. 4Ingieni malangoni mwake kwa shukrani na katika nyua zake kwa kusifu, mshukuruni yeye na kulisifu jina lake. 5Kwa maana Bwana ni mwema na upendo wake wadumu milele; uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.