Mithali 31:3
Proverbs 31:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Usitumie nguvu zako kwa wanawake, uhodari wako kwa wale wanaowaharibu wafalme.
Proverbs 31:3 in English
Proverbs 31:3 · Berean Standard Bible
Do not spend your strength on women or your vigor on those who ruin kings.
Context
1Misemo ya Mfalme Lemueli, usia wa mama yake aliyomfundisha: 2“Ee mwanangu, ee mwana wa tumbo langu,
ee mwana wa nadhiri zangu,* 3Usitumie nguvu zako kwa wanawake,
uhodari wako kwa wale wanaowaharibu wafalme. 4“Ee Lemueli, haifai wafalme,
haifai wafalme kunywa mvinyo,
haifai watawala kutamani sana kileo, 5wasije wakanywa na kusahau vile sheria inavyoamuru
na kuwanyima haki zao wote walioonewa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.