Mithali 27:22
Proverbs 27:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hata ukimtwanga mpumbavu kwenye kinu, ukimtwanga kama nafaka kwa mchi, hutauondoa upumbavu wake.
Proverbs 27:22 in English
Proverbs 27:22 · Berean Standard Bible
Though you grind a fool like grain with mortar and a pestle, yet his folly will not depart from him.
Context
20Kuzimu na Uharibifu havishibi
kadhalika macho ya mwanadamu. 21Kalibu ni kwa ajili ya fedha
na tanuru kwa ajili ya dhahabu,
bali mtu hupimwa kwa sifa azipokeazo. 22Hata ukimtwanga mpumbavu kwenye kinu,
ukimtwanga kama nafaka kwa mchi,
hutauondoa upumbavu wake. 23Hakikisha kuwa unajua hali ya makundi yako
ya kondoo na mbuzi,
angalia kwa bidii ngʼombe zako. 24Kwa kuwa utajiri haudumu milele,
nayo taji haidumu vizazi vyote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.