Mithali 26:14
Proverbs 26:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kama vile mlango ugeukavyo kwenye bawaba zake, ndivyo mvivu ajigeuzavyo kitandani mwake.
Proverbs 26:14 in English
Proverbs 26:14 · Berean Standard Bible
As a door turns on its hinges, so the slacker turns on his bed.
Context
12Je, unamwona mtu ajionaye mwenye hekima
machoni pake mwenyewe?
Liko tumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko kwake. 13Mvivu husema, “Yuko simba barabarani,
simba mkali anazunguka mitaa!” 14Kama vile mlango ugeukavyo kwenye bawaba zake,
ndivyo mvivu ajigeuzavyo kitandani mwake. 15Mtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani,
naye huchoka kuupeleka kwenye kinywa chake. 16Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake mwenyewe,
kuliko watu saba wawezao kujibu kwa busara.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.