Native Bible

Proverbs 24:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa maana ingawa mtu mwenye haki huanguka mara saba, huinuka tena, lakini waovu huangushwa chini na maafa.

Proverbs 24:16 in English

Proverbs 24:16 · Berean Standard Bible

For though a righteous man may fall seven times, he still gets up; but the wicked stumble in bad times.

Context

14Ujue pia kwamba hekima ni tamu kwa nafsi yako, kama ukiipata, kuna matumaini kwako ya siku zijazo, nalo tumaini lako halitakatiliwa mbali. 15Usivizie kama haramia afanyavyo ili kuyashambulia makao ya mwenye haki, wala usiyavamie makazi yake, 16Kwa maana ingawa mtu mwenye haki huanguka mara saba, huinuka tena, lakini waovu huangushwa chini na maafa. 17Usitazame kwa kufurahia adui yako aangukapo; wakati ajikwaapo, usiruhusu moyo wako ushangilie. 18Bwana asije akaona na kuchukia akaiondoa ghadhabu yake mbali naye.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.