Mithali 23:32
Proverbs 23:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mwishowe huuma kama nyoka na kutia sumu yake kama nyoka mwenye sumu.
Proverbs 23:32 in English
Proverbs 23:32 · Berean Standard Bible
In the end it bites like a snake and stings like a viper.
Context
30Ni hao wakaao sana kwenye mvinyo,
hao waendao kuonja mabakuli ya mvinyo uliochanganywa. 31Usiukodolee macho mvinyo wakati ukiwa mwekundu,
wakati unapometameta kwenye bilauri,
wakati ushukapo taratibu! 32Mwishowe huuma kama nyoka
na kutia sumu yake kama nyoka mwenye sumu. 33Macho yako yataona mambo mageni
na moyo wako kuwazia mambo yaliyopotoka. 34Utakuwa kama alalaye katikati ya bahari,
alalaye juu ya kamba ya merikebu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.