Mithali 23:28
Proverbs 23:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kama mnyangʼanyi, hungojea akivizia, naye huzidisha wasio waaminifu miongoni mwa wanaume.
Proverbs 23:28 in English
Proverbs 23:28 · Berean Standard Bible
Like a robber she lies in wait and multiplies the faithless among men.
Context
26Mwanangu, nipe moyo wako,
macho yako na yafuate njia zangu, 27kwa maana kahaba ni shimo refu
na mwanamke mpotovu ni kisima chembamba. 28Kama mnyangʼanyi, hungojea akivizia,
naye huzidisha wasio waaminifu miongoni mwa wanaume. 29Ni nani mwenye ole?
Ni nani mwenye huzuni?
Ni nani mwenye ugomvi?
Ni nani mwenye malalamiko?
Ni nani aliye na majeraha yasiyo na sababu?
Ni nani mwenye macho mekundu? 30Ni hao wakaao sana kwenye mvinyo,
hao waendao kuonja mabakuli ya mvinyo uliochanganywa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.