Mithali 22:16
Proverbs 22:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yeye amwoneaye maskini ili kujiongezea mali, naye ampaye tajiri zawadi, wote huwa maskini.
Proverbs 22:16 in English
Proverbs 22:16 · Berean Standard Bible
Oppressing the poor to enrich oneself or giving gifts to the rich will surely lead to poverty.
Context
14Kinywa cha mwanamke kahaba ni shimo refu;
yeye aliye chini ya ghadhabu ya Bwana
atatumbukia ndani yake. 15Upumbavu umefungwa ndani ya moyo wa mtoto,
bali fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali naye. 16Yeye amwoneaye maskini ili kujiongezea mali,
naye ampaye tajiri zawadi, wote huwa maskini. 17Tega sikio na usikie misemo ya wenye hekima,
elekeza moyo wako kwenye yale nifundishayo, 18kwa maana inapendeza unapoyahifadhi moyoni mwako
na kuwa nayo yote tayari midomoni mwako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.