Mithali 20:18
Proverbs 20:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Fanya mipango kwa kutafuta mashauri, ukipigana vita, tafuta maelekezo.
Proverbs 20:18 in English
Proverbs 20:18 · Berean Standard Bible
Set plans by consultation, and wage war under sound guidance.
Context
16Chukua vazi la yule awekaye dhamana
kwa ajili ya mgeni;
lishikilie iwe dhamana kama anafanya hivyo
kwa ajili ya mwanamke mpotovu. 17Chakula kilichopatikana kwa hila ni kitamu kwa mwanadamu,
bali huishia na kinywa kilichojaa changarawe. 18Fanya mipango kwa kutafuta mashauri,
ukipigana vita, tafuta maelekezo. 19Maneno ya kusengenya husababisha kutokuaminika,
kwa hiyo mwepuke mtu anayezungumza kupita kiasi. 20Ikiwa mtu atamlaani baba yake au mama yake,
taa yake itazimwa katika giza nene.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.