Mithali 17:4
Proverbs 17:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mtu mwovu husikiliza midomo mibaya; mwongo husikiliza kwa makini ulimi wa madhara.
Proverbs 17:4 in English
Proverbs 17:4 · Berean Standard Bible
A wicked man listens to evil lips; a liar gives ear to a destructive tongue.
Context
2Mtumishi mwenye hekima atatawala juu ya mwana aaibishaye,
naye atashirikiana katika urithi kama mmoja wa hao ndugu. 3Kalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru ni kwa ajili ya dhahabu,
bali Bwana huujaribu moyo. 4Mtu mwovu husikiliza midomo mibaya;
mwongo husikiliza kwa makini ulimi wa madhara. 5Yeye anaye mdhihaki maskini huonyesha dharau kwa Muumba wake;
yeyote afurahiaye maafa hataepuka kuadhibiwa. 6Wana wa wana ni taji la wazee,
nao wazazi ni fahari ya watoto wao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.