Mithali 14:7
Proverbs 14:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kaa mbali na mtu mpumbavu, kwa maana hutapata maarifa katika midomo yake.
Proverbs 14:7 in English
Proverbs 14:7 · Berean Standard Bible
Stay away from a foolish man; you will gain no knowledge from his speech.
Context
5Shahidi mwaminifu hadanganyi,
bali shahidi wa uongo humimina uongo. 6Mwenye mzaha huitafuta hekima na haipati,
bali maarifa huja kwa urahisi kwa anayepambanua. 7Kaa mbali na mtu mpumbavu,
kwa maana hutapata maarifa katika midomo yake. 8Hekima ya mwenye busara ni kufikiria njia zake,
bali upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu. 9Wapumbavu hudhihaki kujirekebisha kutoka dhambi,
bali wema hupatikana miongoni mwa wanyofu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.