Obadia 1:4
Obadiah 1:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ingawa unapaa juu kama tai na kufanya kiota chako kati ya nyota, nitakushusha chini kutoka huko,” asema Bwana.
Obadiah 1:4 in English
Obadiah 1:4 · Berean Standard Bible
Though you soar like the eagle and make your nest among the stars, even from there I will bring you down,” declares the LORD.
Context
2“Angalieni, nitawafanya wadogo miongoni mwa mataifa,
mtadharauliwa kabisa. 3Kiburi cha moyo wako kimekudanganya,
wewe unayeishi katika majabali ya miamba
na kufanya makao yako juu,
wewe unayejiambia mwenyewe,
‘Ni nani awezaye kunishusha chini?’ 4Ingawa unapaa juu kama tai
na kufanya kiota chako kati ya nyota,
nitakushusha chini kutoka huko,”
asema Bwana. 5“Ikiwa wevi wangekuja kwako,
ikiwa wanyangʼanyi wangekujia usiku:
Lo! Tazama ni maafa kiasi gani yangekuwa yanakungojea:
je, si wangeiba tu kiasi ambacho wangehitaji?
Kama wachuma zabibu wangekuja kwako,
je, wasingebakiza zabibu chache? 6Lakini tazama jinsi Esau atakavyotekwa,
jinsi hazina zake zilizofichwa zitatekwa nyara!
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.