Obadia 1:16
Obadiah 1:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kama vile ulivyokunywa juu ya mlima wangu mtakatifu, vivyo hivyo mataifa yote watakunywa mfululizo, watakunywa na kunywa, nao watatoweka kana kwamba hawajawahi kuwepo.
Obadiah 1:16 in English
Obadiah 1:16 · Berean Standard Bible
For as you drank on My holy mountain, so all the nations will drink continually. They will drink and gulp it down; they will be as if they had never existed.
Context
14Usingengoja kwenye njia panda
na kuwaua wakimbizi wao,
wala kuwatoa watu wake waliosalia
katika siku ya shida yao. 15“Siku ya Bwana iko karibu
kwa mataifa yote.
Kama ulivyofanya, nawe utafanyiwa vivyo hivyo,
matendo yako yatakurudia juu ya kichwa chako. 16Kama vile ulivyokunywa juu ya mlima wangu mtakatifu,
vivyo hivyo mataifa yote watakunywa mfululizo,
watakunywa na kunywa,
nao watatoweka kana kwamba hawajawahi kuwepo. 17Lakini katika Mlima Sayuni kutakuwepo
na wale watakaookoka;
nao utakuwa mtakatifu,
nayo nyumba ya Yakobo
itamiliki urithi wake. 18Nyumba ya Yakobo itakuwa moto,
na nyumba ya Yosefu itakuwa mwali wa moto;
nayo nyumba ya Esau itakuwa bua kavu,
nao wataiwasha moto na kuiteketeza.
Hakutakuwa na watakaosalimika
kutoka nyumba ya Esau.”
Bwana amesema.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.