Obadia 1:10
Obadiah 1:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa sababu ya jeuri uliyofanya dhidi ya ndugu yako Yakobo, aibu itakufunika; utaangamizwa milele.
Obadiah 1:10 in English
Obadiah 1:10 · Berean Standard Bible
Because of the violence against your brother Jacob, you will be covered with shame and cut off forever.
Context
8“Katika siku hiyo,” asema Bwana,
“je, sitaangamiza watu wenye hekima wa Edomu,
watu wenye ufahamu katika milima ya Esau? 9Ee Temani, mashujaa wako watatiwa hofu,
kila mmoja katika milima ya Esau
ataangushwa chini kwa kuchinjwa. 10Kwa sababu ya jeuri uliyofanya dhidi ya ndugu yako Yakobo,
aibu itakufunika;
utaangamizwa milele. 11Siku ile ulisimama mbali ukiangalia
wakati wageni walipojichukulia utajiri wake
na watu wa nchi nyingine walipoingia malango yake
wakipiga kura kwa ajili ya Yerusalemu,
ulikuwa kama mmoja wao. 12Usingemdharau ndugu yako
katika siku ya msiba wake,
wala kufurahia juu ya watu wa Yuda
katika siku ya maangamizi yao,
wala kujigamba sana
katika siku ya taabu yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.