Native Bible

Numbers 4:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Hii ndiyo huduma ya koo za Wagershoni wakati wanapofanya kazi na kubeba mizigo.

Numbers 4:24 in English

Numbers 4:24 · Berean Standard Bible

This is the service of the Gershonite clans regarding work and transport:

Context

22“Wahesabu pia Wagershoni kwa jamaa zao na koo zao. 23Wahesabu wanaume wote wenye umri wa miaka thelathini hadi hamsini ambao huja kutumika katika Hema la Kukutania. 24“Hii ndiyo huduma ya koo za Wagershoni wakati wanapofanya kazi na kubeba mizigo. 25Watabeba mapazia ya maskani. Hema la Kukutania, kifuniko chake na kifuniko cha nje cha ngozi za pomboo, mapazia ya maingilio ya Hema la Kukutania, 26mapazia ya ua unaozunguka Maskani na madhabahu, pazia la maingilio, kamba na vifaa vyote vinavyotumika katika huduma yake. Wagershoni watafanya yote yatakiwayo kufanyika na vitu hivi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.