Native Bible

Numbers 28:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

kila mmoja atolewe pamoja na sadaka ya nafaka sehemu ya kumi ya efa* ya unga laini uliochanganywa pamoja na robo ya hini* ya mafuta ya zeituni.

Numbers 28:5 in English

Numbers 28:5 · Berean Standard Bible

along with a tenth of an ephah of fine flour * as a grain offering, mixed with a quarter hin of oil from pressed olives.*

Context

3Waambie: ‘Hii ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto mnayomtolea Bwana: wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja wasio na dosari, kama sadaka ya kawaida ya kuteketezwa kila siku. 4Andaa mwana-kondoo mmoja asubuhi na mwingine jioni, 5kila mmoja atolewe pamoja na sadaka ya nafaka sehemu ya kumi ya efa* ya unga laini uliochanganywa pamoja na robo ya hini* ya mafuta ya zeituni. 6Hii ni sadaka ya kawaida ya kuteketezwa iliyoanzishwa katika Mlima Sinai kama harufu nzuri ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto. 7Sadaka ya kinywaji itakayotolewa pamoja na kila mwana-kondoo ni robo ya hini ya kinywaji kilichochachuka. Mimina sadaka ya kinywaji kwa Bwana mahali patakatifu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.