Hesabu 28:6
Numbers 28:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hii ni sadaka ya kawaida ya kuteketezwa iliyoanzishwa katika Mlima Sinai kama harufu nzuri ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto.
Numbers 28:6 in English
Numbers 28:6 · Berean Standard Bible
This is a regular burnt offering established at Mount Sinai as a pleasing aroma, an offering made by fire to the LORD.
Context
4Andaa mwana-kondoo mmoja asubuhi na mwingine jioni, 5kila mmoja atolewe pamoja na sadaka ya nafaka sehemu ya kumi ya efa* ya unga laini uliochanganywa pamoja na robo ya hini* ya mafuta ya zeituni. 6Hii ni sadaka ya kawaida ya kuteketezwa iliyoanzishwa katika Mlima Sinai kama harufu nzuri ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto. 7Sadaka ya kinywaji itakayotolewa pamoja na kila mwana-kondoo ni robo ya hini ya kinywaji kilichochachuka. Mimina sadaka ya kinywaji kwa Bwana mahali patakatifu. 8Andaa yule mwana-kondoo wa pili jioni, pamoja na sadaka ya nafaka na sadaka ya kinywaji kama ulivyofanya kwa ile sadaka nyingine ya asubuhi. Hii ni sadaka iliyotolewa kwa kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.