Hesabu 28:3
Numbers 28:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Waambie: ‘Hii ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto mnayomtolea Bwana: wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja wasio na dosari, kama sadaka ya kawaida ya kuteketezwa kila siku.
Numbers 28:3 in English
Numbers 28:3 · Berean Standard Bible
And tell them that this is the offering made by fire you are to present to the LORD as a regular burnt offering each day: two unblemished year-old male lambs.
Context
1Bwana akamwambia Mose, 2“Wape Waisraeli agizo hili na uwaambie: ‘Hakikisheni kwamba mnaniletea mimi kwa wakati uliowekwa chakula kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa moto, kama harufu nzuri ya kupendeza.’ 3Waambie: ‘Hii ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto mnayomtolea Bwana: wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja wasio na dosari, kama sadaka ya kawaida ya kuteketezwa kila siku. 4Andaa mwana-kondoo mmoja asubuhi na mwingine jioni, 5kila mmoja atolewe pamoja na sadaka ya nafaka sehemu ya kumi ya efa* ya unga laini uliochanganywa pamoja na robo ya hini* ya mafuta ya zeituni.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.