Hesabu 26:56
Numbers 26:56 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kila urithi utagawanywa kwa kura miongoni mwa makundi makubwa na madogo.”
Numbers 26:56 in English
Numbers 26:56 · Berean Standard Bible
Each inheritance is to be divided by lot among the larger and smaller tribes.”
Context
54Kundi kubwa zaidi lipe urithi mkubwa zaidi, na kundi dogo zaidi lipewe urithi mdogo zaidi; kila kundi litapokea urithi wake kulingana na hesabu ya wale walioorodheshwa. 55Hakikisha kuwa nchi inagawanywa kwa kura. Kile kitakachorithiwa na kila kikundi kitakuwa kwa kulingana na majina ya kabila la babu yao. 56Kila urithi utagawanywa kwa kura miongoni mwa makundi makubwa na madogo.” 57Hawa walikuwa Walawi ambao walihesabiwa kwa koo zao:
kutoka kwa Gershoni, ukoo wa Wagershoni;
kutoka kwa Kohathi, ukoo wa Wakohathi;
kutoka kwa Merari, ukoo wa Wamerari. 58Hizi pia zilikuwa koo za Walawi:
ukoo wa Walibni;
ukoo wa Wahebroni;
ukoo wa Wamahli;
ukoo wa Wamushi;
ukoo wa wana wa Kora.
(Kohathi alikuwa baba aliyemzaa Amramu;
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.