Hesabu 16:45
Numbers 16:45 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Jitenge mbali na kusanyiko hili ili niweze kuwaangamiza mara moja.” Wakaanguka chini kifudifudi.
Numbers 16:45 in English
Numbers 16:45 · Berean Standard Bible
“Get away from this congregation so that I may consume them in an instant.” And Moses and Aaron fell facedown.
Context
43Ndipo Mose na Aroni wakaenda mbele ya Hema la Kukutania, 44naye Bwana akamwambia Mose, 45“Jitenge mbali na kusanyiko hili ili niweze kuwaangamiza mara moja.” Wakaanguka chini kifudifudi. 46Kisha Mose akamwambia Aroni, “Chukua chetezo chako na uweke uvumba ndani yake, pamoja na moto kutoka madhabahuni, nawe uende haraka kwenye kusanyiko ili kufanya upatanisho kwa ajili yao. Ghadhabu imekuja kutoka kwa Bwana, na tauni imeanza.” 47Hivyo Aroni akafanya kama Mose alivyosema, akakimbilia katikati ya kusanyiko. Tauni ilikuwa tayari imeanza miongoni mwa watu, lakini Aroni akafukiza uvumba na kufanya upatanisho kwa ajili yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.