Native Bible

Nehemiah 6:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Alikuwa ameajiriwa kunitisha ili kwa kufanya jambo hili nitende dhambi, kisha waweze kuniharibia jina langu na kuniaibisha.

Nehemiah 6:13 in English

Nehemiah 6:13 · Berean Standard Bible

He had been hired to intimidate me so that I would sin by doing as he suggested, so they could give me a bad name in order to discredit me.

Context

11Lakini nikasema, “Je, mtu kama mimi akimbie? Au mtu kama mimi aende Hekaluni kuokoa maisha yake? Sitakwenda!” 12Nilitambua kwamba Mungu hakumtuma, bali alitabiri dhidi yangu kwa sababu Tobia na Sanbalati walikuwa wamemwajiri. 13Alikuwa ameajiriwa kunitisha ili kwa kufanya jambo hili nitende dhambi, kisha waweze kuniharibia jina langu na kuniaibisha. 14Ee Mungu wangu, wakumbuke Tobia na Sanbalati kwa sababu ya yale waliyotenda. Pia kumbuka nabii mke Noadia na manabii wengine ambao wamekuwa wakijaribu kunitisha. 15Basi ukuta ukakamilika siku ya ishirini na tano mwezi wa Eluli,* kazi ambayo ilichukua siku hamsini na mbili.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.