Nehemia 3:22
Nehemiah 3:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Baada yake, ukarabati ulifanywa na makuhani waliotoka eneo lililouzunguka mji.
Nehemiah 3:22 in English
Nehemiah 3:22 · Berean Standard Bible
And next to him, the priests from the surrounding area made repairs.
Context
20Baada yake, Baruku mwana wa Zakai alikarabati kwa bidii sehemu nyingine kuanzia ile pembe, mpaka kwenye lango la nyumba ya Eliashibu kuhani mkuu. 21Kupakana naye, Meremothi mwana wa Uria, mwana wa Hakosi, alikarabati sehemu nyingine, kuanzia penye lango la nyumba ya Eliashibu mpaka mwisho wake. 22Baada yake, ukarabati ulifanywa na makuhani waliotoka eneo lililouzunguka mji. 23Baada yao Benyamini na Hashubu walikarabati mbele ya nyumba zao, na baada yao Azaria mwana wa Maaseya, mwana wa Anania alifanya ukarabati kando ya nyumba yake. 24Baada yake, Binui mwana wa Henadadi alikarabati sehemu nyingine, kuanzia kwenye nyumba ya Azaria mpaka kwenye pembe ya ukuta.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.