Nehemia 3:20
Nehemiah 3:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Baada yake, Baruku mwana wa Zakai alikarabati kwa bidii sehemu nyingine kuanzia ile pembe, mpaka kwenye lango la nyumba ya Eliashibu kuhani mkuu.
Nehemiah 3:20 in English
Nehemiah 3:20 · Berean Standard Bible
Next to him, Baruch son of Zabbai diligently repaired another section, from the angle to the doorway of the house of Eliashib the high priest.
Context
18Baada yake, ukarabati ulifanywa na ndugu zao chini ya usimamizi wa Binui mwana wa Henadadi, mtawala wa nusu hiyo ingine ya wilaya ya Keila. 19Baada yao, Ezeri mwana wa Yeshua, mtawala wa Mispa, alikarabati sehemu nyingine, kuanzia ile sehemu inayotazamana na mwinuko wa kuelekea kwenye ghala la kuhifadhia silaha, mpaka kwenye pembe ya ukuta. 20Baada yake, Baruku mwana wa Zakai alikarabati kwa bidii sehemu nyingine kuanzia ile pembe, mpaka kwenye lango la nyumba ya Eliashibu kuhani mkuu. 21Kupakana naye, Meremothi mwana wa Uria, mwana wa Hakosi, alikarabati sehemu nyingine, kuanzia penye lango la nyumba ya Eliashibu mpaka mwisho wake. 22Baada yake, ukarabati ulifanywa na makuhani waliotoka eneo lililouzunguka mji.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.