Native Bible

Nehemiah 3:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Baada yake, ukarabati ulifanywa na ndugu zao chini ya usimamizi wa Binui mwana wa Henadadi, mtawala wa nusu hiyo ingine ya wilaya ya Keila.

Nehemiah 3:18 in English

Nehemiah 3:18 · Berean Standard Bible

Next to him, their countrymen made repairs under Binnui * son of Henadad, ruler of the other half-district of Keilah.

Context

16Baada yake, Nehemia mwana wa Azbuki, mtawala wa nusu ya wilaya ya Beth-Suri, alikarabati kufikia mkabala na makaburi ya Daudi, mpaka kwenye bwawa lililotengenezwa, na kufikia Nyumba ya Mashujaa. 17Baada yake, ukarabati ulifanywa na Walawi chini ya uongozi wa Rehumu mwana wa Bani. Aliyefuatia ni Hashabia, mtawala wa nusu ya wilaya ya Keila, aliyekarabati sehemu ya wilaya yake. 18Baada yake, ukarabati ulifanywa na ndugu zao chini ya usimamizi wa Binui mwana wa Henadadi, mtawala wa nusu hiyo ingine ya wilaya ya Keila. 19Baada yao, Ezeri mwana wa Yeshua, mtawala wa Mispa, alikarabati sehemu nyingine, kuanzia ile sehemu inayotazamana na mwinuko wa kuelekea kwenye ghala la kuhifadhia silaha, mpaka kwenye pembe ya ukuta. 20Baada yake, Baruku mwana wa Zakai alikarabati kwa bidii sehemu nyingine kuanzia ile pembe, mpaka kwenye lango la nyumba ya Eliashibu kuhani mkuu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.