Native Bible

Nehemiah 3:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Baada yake, Nehemia mwana wa Azbuki, mtawala wa nusu ya wilaya ya Beth-Suri, alikarabati kufikia mkabala na makaburi ya Daudi, mpaka kwenye bwawa lililotengenezwa, na kufikia Nyumba ya Mashujaa.

Nehemiah 3:16 in English

Nehemiah 3:16 · Berean Standard Bible

Beyond him, Nehemiah son of Azbuk, ruler of a half-district of Beth-zur, made repairs up to a point opposite the tombs of David, as far as the artificial pool and the House of the Mighty.

Context

14Lango la Samadi lilikarabatiwa na Malkiya mwana wa Rekabu, mtawala wa wilaya ya Beth-Hakeremu. Alilijenga upya, na kuweka milango yake, na makomeo na nondo. 15Lango la Chemchemi lilikarabatiwa na Shalumu mwana wa Kolhoze, mtawala wa wilaya ya Mispa. Alilijenga upya, akaliezeka na kuweka milango yake, na makomeo na nondo mahali pake. Pia alikarabati ukuta wa Bwawa la Siloamu karibu na Bustani ya Mfalme, hadi kwenye ngazi zinazoshuka kutoka Mji wa Daudi. 16Baada yake, Nehemia mwana wa Azbuki, mtawala wa nusu ya wilaya ya Beth-Suri, alikarabati kufikia mkabala na makaburi ya Daudi, mpaka kwenye bwawa lililotengenezwa, na kufikia Nyumba ya Mashujaa. 17Baada yake, ukarabati ulifanywa na Walawi chini ya uongozi wa Rehumu mwana wa Bani. Aliyefuatia ni Hashabia, mtawala wa nusu ya wilaya ya Keila, aliyekarabati sehemu ya wilaya yake. 18Baada yake, ukarabati ulifanywa na ndugu zao chini ya usimamizi wa Binui mwana wa Henadadi, mtawala wa nusu hiyo ingine ya wilaya ya Keila.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.