Nehemia 13:12
Nehemiah 13:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yuda wote walileta zaka za nafaka, divai mpya na mafuta kwenye ghala.
Nehemiah 13:12 in English
Nehemiah 13:12 · Berean Standard Bible
and all Judah brought a tenth of the grain, new wine, and oil into the storerooms.
Context
10Pia niligundua kuwa mafungu yaliyopangwa kupewa Walawi hawakuwa wamepewa, nao Walawi wote na waimbaji waliowajibika kwa huduma walikuwa wamerudi katika mashamba yao. 11Basi niliwakemea maafisa na kuwauliza, “Kwa nini nyumba ya Mungu imepuuzwa?” Kisha niliwaita pamoja na kuwaweka kwenye nafasi zao. 12Yuda wote walileta zaka za nafaka, divai mpya na mafuta kwenye ghala. 13Nikamweka kuhani Shelemia, mwandishi Sadoki, na Mlawi aliyeitwa Pedaya kuwa wasimamizi wa ghala, na kumfanya Hanani mwana wa Zakuri, mwana wa Matania kuwa msaidizi wao, kwa sababu watu hawa walionekana kuwa waaminifu. Walipewa wajibu wa kugawa mahitaji kwa ndugu zao. 14Ee Mungu wangu, unikumbuke kwa hili, wala usifute kile nilichokifanya kwa uaminifu kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu na kwa ajili ya huduma yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.