Native Bible

Nehemiah 1:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hanani, mmoja wa ndugu zangu, alikuja kutoka Yuda akiwa na watu wengine, nami nikawauliza kuhusu mabaki ya Wayahudi wale walionusurika kwenda uhamishoni na pia kuhusu Yerusalemu.

Nehemiah 1:2 in English

Nehemiah 1:2 · Berean Standard Bible

Hanani, one of my brothers, arrived with men from Judah. So I questioned them about the remnant of the Jews who had survived the exile, and also about Jerusalem.

Context

1Maneno ya Nehemia mwana wa Hakalia: Katika mwezi wa Kisleu* katika mwaka wa ishirini, wakati nilikuwa ngomeni katika jumba la kifalme la Shushani, 2Hanani, mmoja wa ndugu zangu, alikuja kutoka Yuda akiwa na watu wengine, nami nikawauliza kuhusu mabaki ya Wayahudi wale walionusurika kwenda uhamishoni na pia kuhusu Yerusalemu. 3Wakaniambia, “Wale walionusurika kwenda uhamishoni, wale ambao wamerudi kwenye lile jimbo, wako katika taabu kubwa na aibu. Ukuta wa Yerusalemu umebomoka, na malango yake yamechomwa moto.” 4Niliposikia mambo haya, niliketi, nikalia. Kwa siku kadhaa niliomboleza na kufunga na kuomba mbele za Mungu wa mbinguni.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.