Nahumu 3:2
Nahum 3:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kelele za mijeledi, vishindo vya magurudumu, farasi waendao mbio na mshtuo wa magari ya vita!
Nahum 3:2 in English
Nahum 3:2 · Berean Standard Bible
The crack of the whip, the rumble of the wheel, galloping horse and bounding chariot!
Context
1Ole wa mji umwagao damu,
uliojaa uongo,
umejaa nyara,
usiokosa kuwa na vitu vya kuteka nyara. 2Kelele za mijeledi,
vishindo vya magurudumu,
farasi waendao mbio
na mshtuo wa magari ya vita! 3Wapanda farasi wanaenda mbio,
panga zinameremeta,
na mikuki inangʼaa!
Majeruhi wengi,
malundo ya maiti,
idadi kubwa ya miili isiyohesabika,
watu wanajikwaa juu ya mizoga: 4yote haya kwa sababu ya wingi wa tamaa za kahaba,
anayeshawishi, bibi wa mambo ya uchawi,
anayewatia utumwani mataifa kwa ukahaba wake
na pia jamaa za watu kwa ulozi wake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.