Nahumu 3:18
Nahum 3:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ee mfalme wa Ashuru, wachungaji wako wanasinzia; wakuu wako wanalala chini mavumbini kupumzika. Watu wako wametawanyika juu ya milima bila kuwa na mtu yeyote wa kuwakusanya.
Nahum 3:18 in English
Nahum 3:18 · Berean Standard Bible
O king of Assyria, your shepherds slumber; your officers sleep. Your people are scattered on the mountains with no one to gather them.
Context
16Umeongeza idadi ya wafanyabiashara wako
mpaka wamekuwa wengi kuliko nyota za angani,
lakini kama nzige wanaacha nchi tupu
kisha huruka na kwenda zake. 17Walinzi wako ni kama nzige,
maafisa wako ni kama makundi ya nzige
watuao kwenye kuta wakati wa siku ya baridi:
lakini wakati jua linapotokea wanaruka kwenda zao,
na hakuna ajuaye waendako. 18Ee mfalme wa Ashuru, wachungaji wako wanasinzia;
wakuu wako wanalala chini mavumbini kupumzika.
Watu wako wametawanyika juu ya milima
bila kuwa na mtu yeyote wa kuwakusanya. 19Hakuna kitu kinachoweza kuponya jeraha lako;
jeraha lako ni la kukuua.
Kila anayesikia habari zako,
hupiga makofi kwa kuanguka kwako,
kwa kuwa ni nani ambaye hajaguswa
na ukatili wako usio na mwisho?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.