Marko 9:16
Mark 9:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akawauliza wanafunzi wake, “Mnabishana nao kuhusu nini?”
Mark 9:16 in English
Mark 9:16 · Berean Standard Bible
“What are you disputing with them?” He asked.
Context
14Walipowafikia wale wanafunzi wengine, wakawakuta wamezungukwa na umati mkubwa wa watu na baadhi ya walimu wa sheria wakibishana nao. 15Mara wale watu walipomwona Yesu, wakastaajabu sana, wakamkimbilia ili kumsalimu. 16Akawauliza wanafunzi wake, “Mnabishana nao kuhusu nini?” 17Mtu mmoja miongoni mwa ule umati wa watu akajibu, “Mwalimu, nilimleta kwako mwanangu ambaye ana pepo mchafu anayemfanya asiweze kuongea. 18Kila mara huyo pepo mchafu ampagaapo mwanangu, humwangusha chini na kumfanya atokwe povu mdomoni na kusaga meno, kisha mwili wake hukauka. Niliwaomba wanafunzi wako wamtoe huyo pepo mchafu, lakini hawakuweza.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.