Native Bible

Mark 9:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Walipowafikia wale wanafunzi wengine, wakawakuta wamezungukwa na umati mkubwa wa watu na baadhi ya walimu wa sheria wakibishana nao.

Mark 9:14 in English

Mark 9:14 · Berean Standard Bible

When they returned to the other disciples, they saw a large crowd around them, and scribes arguing with them.

Context

12Yesu akawajibu, “Ni kweli, Eliya yuaja kwanza ili kutengeneza mambo yote. Mbona basi imeandikwa kwamba Mwana wa Adamu ni lazima ateseke sana na kudharauliwa? 13Lakini ninawaambia, Eliya amekwisha kuja, nao wakamtendea walivyopenda, kama ilivyoandikwa kumhusu yeye.” 14Walipowafikia wale wanafunzi wengine, wakawakuta wamezungukwa na umati mkubwa wa watu na baadhi ya walimu wa sheria wakibishana nao. 15Mara wale watu walipomwona Yesu, wakastaajabu sana, wakamkimbilia ili kumsalimu. 16Akawauliza wanafunzi wake, “Mnabishana nao kuhusu nini?”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.