Marko 9:17
Mark 9:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mtu mmoja miongoni mwa ule umati wa watu akajibu, “Mwalimu, nilimleta kwako mwanangu ambaye ana pepo mchafu anayemfanya asiweze kuongea.
Mark 9:17 in English
Mark 9:17 · Berean Standard Bible
Someone in the crowd replied, “Teacher, I brought You my son, who has a spirit that makes him mute.
Context
15Mara wale watu walipomwona Yesu, wakastaajabu sana, wakamkimbilia ili kumsalimu. 16Akawauliza wanafunzi wake, “Mnabishana nao kuhusu nini?” 17Mtu mmoja miongoni mwa ule umati wa watu akajibu, “Mwalimu, nilimleta kwako mwanangu ambaye ana pepo mchafu anayemfanya asiweze kuongea. 18Kila mara huyo pepo mchafu ampagaapo mwanangu, humwangusha chini na kumfanya atokwe povu mdomoni na kusaga meno, kisha mwili wake hukauka. Niliwaomba wanafunzi wako wamtoe huyo pepo mchafu, lakini hawakuweza.” 19Yesu akawaambia, “Enyi kizazi kisicho na imani! Nitakuwa pamoja nanyi mpaka lini? Nitawavumilia mpaka lini? Mleteni mvulana kwangu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.