Native Bible

Mark 8:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wanafunzi wake wakamjibu, “Lakini hapa nyikani tutapata wapi mikate ya kutosha kuwalisha?”

Mark 8:4 in English

Mark 8:4 · Berean Standard Bible

His disciples replied, “Where in this desolate place could anyone find enough bread to feed all these people?”

Context

2“Ninauhurumia huu umati wa watu, kwa sababu sasa wamekuwa nami kwa muda wa siku tatu na hawana chakula. 3Nikiwaaga waende nyumbani bila kula, watazimia njiani kwa sababu baadhi yao wametoka mbali.” 4Wanafunzi wake wakamjibu, “Lakini hapa nyikani tutapata wapi mikate ya kutosha kuwalisha?” 5Yesu akawauliza, “Mna mikate mingapi?” Wakajibu, “Tuna mikate saba.” 6Akawaambia watu waketi chini. Akiisha kuichukua mikate saba na kushukuru, akaimega na kuwapa wanafunzi wake ili wawagawie watu. Wanafunzi wake wakafanya hivyo.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.